ZURA YAKAGUA VISIMA VYA MAJI WILAYA YA WETE PEMBA

ZURA YAKAGUA VISIMA VYA MAJI WILAYA YA WETE PEMBA

Mamlaka ya Udhibiti ya Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya ukaguzi wa changamoto ya Umeme mdogo katika visima vya maji katika Wilaya ya Wete Pemba.

Mamlaka imefanya ukaguzi huo leo tarehe 07 Mei 2024 kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) katika maeneo ya Kwale Gongo, Taifu na Weni Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Ukaguzi huo umejikita  zaidi katika kukagua visima vya Maji ili kuondoa changamoto ya Umeme mdogo wa visima kwa Wilaya hyio ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya maji kwa wakati.

ZURA imeitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuimarisha ulinzi muda wote katika visima hivyo ili kuzuia kutokea wizi au uharibifu wowote.

Mamlaka hufanya ukaguzi wa vyanzo na miundombinu ya Maji mara kwa mara Unguja na Pemba ili kuhakikisha huduma ya maji inayotolewa inakuwa katika hali ya usalama.