Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imeshiriki katika Maonesho ya Marashi ya Karafuu ya Wajasiriamali wa Kisiwa cha Pemba.
Maonesho hayo yanayofanyika Gombani Pemba kuanzia Tarehe 23/02/2024 mpaka Tarehe 25/02/2024 yamefunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusimi Pemba Mhe. Mattar Zahor Massoud.
Mamlaka imeshiriki katika Maonesho hayo ili kuunga mkono juhudi za Wajasiriamali hao ambao ni watumiaji wakubwa wa huduma zote zinazodhibitiwa na Mamlaka, ambapo pia Mamlaka itapata fursa ya kutoa elimu kwa Wananchi watakaotembelea katika Maonesho hayo.
Aidha, pamoja na elimu inayotolewa kwa wananchi katika maonesho hayo, pia Mamlaka itapata fursa nzuri ya kuongeza idadi ya wawekezaji katika Sekta za Maji na Nishati kwa wawekezaji watakaotembelea maonesho hayo.