ZURA YASHIRIKI MAONESHO YA KUMI YA BIASHARA

ZURA YASHIRIKI MAONESHO YA KUMI YA BIASHARA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati imeshiriki maonesho ya kumi ya biashara yanayofanyika Nyamanzi Zanzibar kuanzia Tarehe 07/01/2024 mpaka Tarehe 19/01/2024.

Ushiriki katika Maonesho hayo Mamlaka itapata fursa ya kutoa elimu kwa wadau wake wote watakaotembelea katika banda la Mamlaka.

Aidha, pamoja na elimu inayotolewa kwa wananchi katika maonesho hayo pia Mamlaka itapata fursa nzuri ya kuongeza idadi ya wawekezaji katika Sekta za Maji na Nishati kwa vile wawekezaji hao hutembelea na kuweza kujua juu ya uekezaji katika sekta hizo.

ZURA imekua ni mshiriki mkubwa wa maonesho, na kuhamashisha uwekezaji katika sekta ya Mafuta Maji ,Umeme na Gesi.