ZURA YASHIRIKI KATIKA HAFLA YA UGAWAJI WA MITUNGI YA GESI YA KUPIKIA VIJIJINI MKOA WA KUSINI UNGUJA.

ZURA YASHIRIKI KATIKA HAFLA YA UGAWAJI WA MITUNGI YA GESI YA KUPIKIA VIJIJINI MKOA WA KUSINI UNGUJA.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati imeshiriki katika hafla ya Ugawaji wa Mitungi ya Gesi iliyoandaliwa na Kampuni ya Orxy chini ya udhamini wa Mradi wa kuwawezesha wanawake na Vijijini kiuchumi (FAWE) iliyofanyika Tarehe 19/12/2023 maeneo ya Dunga Skuli Zanzibar.

Aidha hafla hiyo ilifunguliwa na Mgeni Rasmi Waziri wa Maji, Nishati na Madini (WMNM) Mhe. Shaibu Hassan Kaduwara Alieleza kuwa waingizaji wa Gesi na wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano kama huu katika kuwawezesha wanawake vijijini kutumia nishati ya gesi ya kupikia LPG kwa kuachana na nishati isiyo sahihi kama kuni ambayo itapelekea athari za kiafya kwa Jamii.

ZURA kwa kushirikiana na FAWE Pamoja na kushirikiana na kampuni ya Orxy wamegawa Mitungi 350 kwa wanakijiji kutoka Uroa, Chwaka, Jambiani, Uzi na Uzi ng’abwa ambapo katika hiyo Mitungi Mia 100 ni wadhamini kutoka Zura.

Ushiriki katika hafla hiyo Mamlaka imepata fursa ya kutoa elimu juu ya huduma zinazodhibitiwa zikiwemo Maji, Umeme, Mafuta Pamoja na Gesi ya Kupikia.

Kampuni ya Orxy ipo katika hatuwa za Mwisho za Ujenzi wa miundombino ya Meli ya kupokeai ya Gesi na kuongeza Matangi mawili ya kuhefadhia Gesi yenye ujazo wa Metrik ton (650) na unotarajiwa kumaliza Mwezi wa Pili 2024 hali hii itachochea kupunguza ukali wa Bei ya Gesi ya Kupikia Zanzibar.