ZURA YAFANYA KIKAO KIFUPI NA ZBC KUIMARISHA USHIRIKIANO BAINA YAO.

ZURA YAFANYA KIKAO KIFUPI NA ZBC KUIMARISHA USHIRIKIANO BAINA YAO.

Mkurugenzi Mkuu ZURA Ndg. Omar Ali Yussuf pamoja na watendaji wake wa Kitengo cha Uhusiano amefanya Kikao kifupi na Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Ndg. Ramadhan Bukini akiambatana na watendaji wake.

Lengo la kikao hicho ni kujadili kwa pamoja namna ya kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Taasisi hizo mbili ili kuchochea Maendeleo ya Zanzibar.

Aidha, Kikao hicho kiliazimia kuongeza ushirikiano ili kuzitangaza kwa jamii Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na Mamlaka.

Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za ZURA Maisara Leo Tarehe 20/12/2023.