ZURA YAPOKEA CHETI CHA SHUKRANI KWA UDHAMINI WA TIMU YA TAIFA ZANZIBAR KATIKA MASHINDANO YA CECAFA U-15

ZURA YAPOKEA CHETI CHA SHUKRANI KWA UDHAMINI WA TIMU YA TAIFA ZANZIBAR KATIKA MASHINDANO YA CECAFA U-15

Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Ndg. Omar Ali Yussuf amepokea Cheti cha Shukrani kwa kuchangia Timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya Miaka 15 (Karume Boys) TZS 2,500,000.

Cheti hicho kilikabidhiwa na Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar, Ndg. Abubakar Lunda akiambatana na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) katika Ofisi za ZURA Leo Tarehe 15/12/2023, Maisara Zanzibar.

Akipokea Cheti hiyo Mkurugenzi Mkuu ZURA aliahidi kuendelea kuwaunga mkono kwa kuchangia Vyama vya Michezo ili kukuza na kuimarisha Michezo ili kuendana na Adhma ya Rais wa Zanziabr Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya Miaka 15 (Karume Boys) ilishiriki Mashindano ya Vijana U-15 ya CECAFA yaliyofanyika Nchini Uganda na Kutwaa Ubingwa wa Mashindano hayo.