ZURA YASHIRIKI TAMASHA LA UTALII PEMBA

ZURA YASHIRIKI TAMASHA LA UTALII PEMBA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imeshiriki katika Tamasha la Utalii Pemba lilofunguliwa na Mgeni Raismi Mwenyekiti wa Bodi wa Kamisheni ya Utalii Ndg. Ibrahim Baloo. Tamasha hilo limefunguliwa leo Tumbe Tarehe 28/11/2023 litakaloendelea mpaka Tarehe 03/11/2023.

Tamasha hilo limekusanya shughuli za kiutamaduni na michezo mbalimbali yakiwemo Mchezo wa Bao, mashindano ya Ngalawa,usafishwaji wa fukwe, Mashindano ya dufu, Mchezo wa ng’ombe, na Mashindano ya kuogelea. Lengo kuu la tamasha hilo ni kukuza ongezeko la watalii kisiwani pemba

Wadau walioshiriki katika Tamasha hiyo ni ZURA, ASAS, ZRA, Mozet Tours and Safari, Safina Tours, Adventure, Safina Get Away, ZSTC, Baraza la Michezo, International Sport Festival, Mozeti Tour, Dege Adventure na KVZ.

Ushiriki katika Tamasha hilo itaipa Mamlaka fursa ya kuweza kutoa elimu kwa wadau wake wote watakaotembelea katika Maoneo hayo kuweza kupata elimu juu ya huduma zinazodhibitiwa zikiwemo Maji, Umeme, Mafuta pamoja na Gesi ya kupikia (LPG).

Aidha, pamoja na elimu inayotolewa kwa wananchi katika Tamasha hilo pia Mamlaka itapata fursa nzuri ya kuongeza idadi ya wawekezaji katika Sekta za Maji na Nishati kwa vile wawekezaji hao hutembelea na kuweza kujua juu ya uekezaji katika sekta hizo.

ZURA imekua ni miongoni mwa washiriki katika Tamasha La Utalii Pemba ikizingatiwa kuwa wadau wengi katika sekta ya Utalii wanategemea sana Huduma za Maji na Nishati kwa ajili ya kuendeleza Shughuli zao za kila siku