ZURA YASHIRIKI KATIKA WARSHA YA WADAU WA NISHATI.

ZURA YASHIRIKI KATIKA WARSHA YA WADAU WA NISHATI.

Mamlaka ya Udhibiti Huduma Za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imeshiriki warsha ya wadau wa maendeleo katika sekta ya nishati kupitia Mradi wa Mabadiliko ya sekta ya nishati na ufikiwaji wa Huduma ya Umeme Zanzibar (ZESTA) uliopo chini ya Udhamini na Benki kuu ya Dunia Chini ya Usimamizi wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar (WMNM).

Warsha hiyo imefanyika Tarehe 15/11/2023 katika Hoteli ya Verde Zanzibar na ilifunguliwa na Mgeni Rasmin Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini (WMNM) Mhe. Shabani Ali Othman alieleza kuwa mashirikiano kwa wadau wa nishati yataleta mabadiliko makubwa katika maendeleo ya Sekta za Umeme, Mafuta pamoja na Gesi.

Aidha, wadau walioshiriki katika warsha hiyo wakiwemo Viongozi kutoka Wizara ya Maji Nishati na Madini (WMNM), Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA), Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Wold Benk, Jika, Usaid, IFC na Norad.

Baada ya warsha hiyo ZURA ilipata fursa ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi na Uimarishaji wa miundombinu ya kusambaza umeme baina ya ZECO na Kampuni ya WPCOS kutoka India.