ZURA YAFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME WILAYA YA KATI MKOA WA KUSINI UNGUJA

ZURA YAFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME WILAYA YA KATI MKOA WA KUSINI UNGUJA

Mamlaka ya Udhibiti ya Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya ukaguzi wa ubora wa huduma ya Umeme kwa kukagua Transfoma za usambazaji wa Umeme majumbani katika Wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja.

Mamlaka kwa kushirikiana na Mtendaji kutoka Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO)imefanya ukaguzi huo tarehe 26/10/2023 katika maeneo mbali mbali ikiwemo Mwera Bango la Mkoa, Mwera Mishoki shokini, Mwera Pongwe, Koani, Kidimni, Dunga Wilayani, Ndijani Skuli, Hanyengwa, Kijundu, Chwaka na Uroa.

Ukaguzi huo umelenga zaidi katika kuhakikisha sehemu za kupokelea umeme mkubwa (HT) katika Transfoma zinakuwa katika mazingira salama na kukagua mfumo wa kiusalama wa waya (Metal Earth and Lightning arrester Earth) pamoja na kuhakikisha alama za tahadhari zimebandikwa katika Transfoma hizo.

Mamlaka imependezwa na juhudi zilizochukuliwa na shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kwa utekelezaji na uboreshaji wa Miundombinu hiyo itakayosaidia upatikanaji wa huduma ya umeme kwa kuzingatia usalama kwa watumiaji.

Mamlaka hufanya ukaguzi wa miundombinu ya Umeme mara kwa mara kwa lengo la kuimarisha huduma ya Umeme ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza katika Transfoma hizo kwa Visiwa vya Unguja na Pemba.