ZURA YAFANYA UKAGUZI WA MAJI WILAYA YA MICHEWENI

ZURA YAFANYA UKAGUZI WA MAJI WILAYA YA MICHEWENI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya ukaguzi wa Miundombinu ya Maji kwa kutembelea Visima viwili na Matangi yanayosambaza Maji yaliyojengwa kwa mradi wa Uviko – 19 matangi mawili hayo ni tangi la kilindi kironjo na Makangale katika Wilaya ya Micheweni Mjini Mkoa wa Kaskazini Pemba, ZURA imefanya ukaguzi huo tarehe 15 Oktoba 2023 kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Pemba katika kisima cha Kirinjo na Makangale. Tangi la Maji liliopo Kilindi Kironjo ambalo linaloendelea kujegwa chini ya mradi huo wa Uviko -19 lina ujazo wa lita 1,000,000 za maji ambazo linatarajia kuhudumia shehia nane (8) katika wilaya ya Micheweni nazo ni Mjini wingwi, Majenzi, Shumba Mjini, Micheweni Mjini, Micheweni Shambini, Maziwang’ombe, Kunju na Shanake, na Tangi la Makangale lenye ujazo wa lita 1,000,000 ambalo linasambaza Maji katika vijiji vya Makangale na Tondoni pamoja na hotel 6. Afisa maji wilaya ya Micheweni Ndg. Yussuf Ali Faki alieleza kuwa Matangi yote Mawili yataweza kuhifadhi maji hayo na kusaidia sana katika kuhakikisha changamoto ya maji katika wilaya ya micheweni yatapungua. Aidha , ZURA imeitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuimarisha ulinzi imara na kuhakikisha Miundombinu inalindwa ipasavyo kwa muda wote. Mamlaka hufanya ukaguzi wa vyanzo na miundombinu ya Maji mara kwa mara Unguja na Pemba ili kuhakikisha Huduma ya Maji inayotolewa inakuwa katika hali ya usalama Zaidi.