ZURA YAFANYA UKAGUZI WA UMEME WA JUA NJAU, PEMBA.

ZURA YAFANYA UKAGUZI WA UMEME WA JUA NJAU, PEMBA.

Mamlaka ya Udhidhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya ukaguzi wa Mradi ya Umeme wa Jua katika Kisiwa cha Najau, Pemba ili kuona maendeleo na hali halisi ya uzalishaji na usambazaji wa huduma ya Umeme katika Kisiwa cha Njau.

Mkaguzi Umeme ZURA Ndg. Abdulla Khamas amepata nafasi ya kujionea hali halisi ya Mradi wa Umeme wa jua unaosimamiwa na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) uliopo katika Kisiwa cha Njau ambao unauwasaidia wananchi wa vijiji hicho kwa matumizi yao ikiwemo kuhifadhia Vitoweo hasa kwavile Uvuvi ndio nshughuli yao kubwa ya kujipatia kipato.

Nae, Fundi wa Mradi huo kutoka ZECO ameeleza kuwa Mradi huo umelenga kunufaisha zaidi ya Wakaazi mia moja (100) wa Kisiwa hicho, na kusisitia kuwa huduma ya Umeme wanayoipata ni endelevu na ya uhakika, ambapo huwa haitokei kukosekana kwa Huduma hiyo.

Aidha, Mamlaka imejiridhisha na imetoa pongezi kwa wazalishaji hao kwa kufuata Kanuni, Miongozo na misingi ya kiusalama katika uzalishaji wa Huduma ya Umeme wa Jua kwa matumizi ya kila siku katika Kisiwa hicho.

Mamlaka hufanya ukaguzi mara kwa mara wa Miundombinu ya Umeme kwa wazalishaji na kuhakikisha wanafuata Kanuni na Miongozo iliyowekwa na Mamlaka ili kuhakikisha watumiaji wanapata huduma stahiki, yenye ubora na kiwango cha juu.