ZURA YASHIRIKI MAONESHO YA CHAKULA CHAMANANGWE PEMBA

ZURA YASHIRIKI MAONESHO YA CHAKULA CHAMANANGWE PEMBA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati imeshiriki maonesho ya Chakula duniani yanayofanyika Chamanangwe Pemba kuanzia Tarehe 10/08/2023 mpaka Tarehe 16/08/2023.
Ushiriki katika Maonesho hayo utaipa Mamlaka fursa ya kuweza kutoa elimu kwa wadau wake wote watakaotembelea katika banda la Mamlaka na kuweza kupata elimu juu ya huduma zinazodhibitiwa zikiwemo Maji, Umeme, Mafuta pamoja na Gesi ya kupikia (LPG). Wananchi hao pia watapata uelewa wa matumizi sahihi na salama ya huduma hizo.
Aidha, pamoja na elimu inayotolewa kwa wananchi katika maonesho hayo pia Mamlaka itapata fursa nzuri ya kuongeza idadi ya wawekezaji katika Sekta za Maji na Nishati kwa vile wawekezaji hao hutembelea na kuweza kujua juu ya uekezaji katika sekta hizo.
ZURA imekua ni miongoni mwa washiriki katika maonesho ya chakula duniani katika maadhimisho ya siku ya chakula ambacho huadhimishwa Tarehe 10 Mwezi 10 kila mwaka, ikizingatiwa kuwa wadau wengi katika sekta ya chakula ni wakulima ambao wantegemea sana kwa ajili ya umwagiliaji (irrigation).