Bei zilizotangazwa kwa Mwezi Oktoba ni kama zifuatazo Petroli TZS 3,001, Dizeli TZS 3,012, Mafuta ya Taa TZS 2,921 na Mafuta ya Ndege TZS 2,768 ambapo kwa Mwezi Septemba 2023 Bei za Mafuta zilikua Petroli TZS 2,950, Dizeli TZS 3,012, Mafuta ya Taa TZS 2,921 na Mafuta ya Ndege TZS 2,448.
Bei hizo zimetangazwa Siku ya Jumapili Tarehe 08/10/2023 katika Ofisi za ZURA zilizopo Maisara na Meneja wa Kitengo cha Uhusiano Ndg. Mbarak Hassan Haji kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu ZURA na kueleza sababu za kuongezeka Bei za Dizeli na Mafuta ya Ndege ni kuongezeka Bei hizo katika soko la Dunia kwa asilimia na gharama za bima na usafirishaji kwa asilimia ikilinganishwa na Mwezi Septemba.
Aidha, Meneja huyo alitaja vigezo vinavyotumika na Mamlaka katika kupanga bei, ambavyo ni Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations), Gharama za uingizaji Mafuta katika Bandari ya Dar-es-Salaam na Tanga, Thamani ya Shilingi ya Tanzania kwa Dola za Kimarekani, Gharama za Usafiri, Bima na ‘Premium’ hadi Zanzibar, Kodi na Tozo za Serikali na Kiwango cha faida kwa Wauzaji wa Jumla na Reja Reja.
Mamlaka hutangaza Bei za Mafuta Tarehe 8 ya kila Mwezi ambapo hutoa wito kwa Wananchi kununua Mafuta katika Vituo halali vya Mafuta na kudai Risiti za Kielektroniki kila wanaponunua Mafuta.