ZURA YAFANYA UKAGUZI WA MAJI WILAYA YA KASKAZINI “A”

ZURA YAFANYA UKAGUZI WA MAJI WILAYA YA KASKAZINI “A”

Mamlaka ya Udhibiti ya Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya ukaguzi wa ubora wa huduma ya Maji kwa kukagua  visima  mbali mbali vya usambazaji wa Maji majumbani katika Wilaya ya Kaskazini “A” .

Mamlaka imefanya ukaguzi huo tarehe 27 Septemba 2023 kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Zanzibar (zawa) katika maeneo mbali mbali ikiwemo Chaani, Kilindi, Kiashangi, Matemwe Mlili na Kandwi.

Ukaguzi huo umejikita  zaidi katika kuboresha na kuimarisha ubora wa maji yanayosambazwa kwa wananchi kuhakikisha yapo katika kiwango (standard ) inayotakiwa nayapo katika mazingira salama kwa watumiaji.

Aidha, ZURA imeitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuimarisha ulinzi imara na kuhakikisha Miundombinu inalindwa ipasavyo kwa muda wote, pia, ZURA  imesisitiza kuwa  itahakikisha ulinzi  katika vyanzo  vya Maji  unaimarishwa ili kuvilinda ipasavyo  vyanzo hivyo na kuzuia kutokea uharibifu .

Mamlaka hufanya ukaguzi wa  vyanzo na miundombinu ya Maji mara kwa mara Unguja na Pemba ili kuhakikisha Huduma ya Maji inayotolewa inakuwa katika hali ya usalama Zaidi