ZURA YATOA MAFUNZO KWA TRA NA ZRA PEMBA.

ZURA YATOA MAFUNZO KWA TRA NA ZRA PEMBA.

Mamlaka ya Udhidbiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA kupitia Afisi ya Pemba imendesha mafunzo ya siku nne (4) kwa Uongozi na Watendaji wa TRA na ZRA ya Ushushaji wa mafuta katika bohari ya Wesha Pemba.

Mafunzo hayo yamejikita zaidi katika suala zima la usimamizi wa zoezi la ushushaji wa mafuta ili kutokomeza njia zisizo rasmi, za ushushaji wa mafuta katika bohari hiyo.

Aidha ZURA imeona ipo haja ya kuandaa mafunzo ya siku nne kwa lengo la kuimarisha njia sahihi za ushushaji wa nishati hiyo zenye manufaa kwa wananchi wa Kisiwan humo.

ZURA imewasisitiza zaidi watendaji wa TRA na ZRA kushiriki kikamilifu katika zoezi la ushushaji wa mafuta na kufuata taratibu za kiufundi na za kiusalama zilizoekwa, pamoja na kuhakiksha kwamba hakuna uvujaji wowote wa mapato ya serkali.

Malaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) kwa kupitia Ofisi ya ZURA Pemba zimeandaa mafunzo hayo ili kuaimarisha mashirikiano na uhusiano uliopo baina ya taasisi hizo.