ZURA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA SKULI KWA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR.

ZURA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA SKULI KWA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetoa msaada wa Vifaa vya Skuli kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA) Zanzibar.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa Afisa Utawala ZURA Ndg. Salum Shomari Salum kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu ZURA kwa lengo kupatiwa wanafunzi ikiwa ni zawadi katika maadhimisho ya siku ya Elimu bila ya Malipo.

Akipokea vifaa hivyo Naibu Katibu Mkuu WEMA Ndg. Mwanahamis Adam Ameir alieleza lengo la vifaa hivyo ni kusaidia Wanafunzi katika mashindano ya Elimu bila ya Malipo na kuwahamisisha katika mahudhurio yao ya Skuli.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Mikoba Thelathini (30), ‘Scientific Calculator’ Tisa (9), Mabuku Mia Nne Themanini (480), Mistari Thelathini (30), Penseli Mia Nne (400).