ZURA YASHIRIKI KONGAMANO NA WAANDISHI KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA ENEO LA MAFUTA NA GESI MANGAPWANI

ZURA YASHIRIKI KONGAMANO NA WAANDISHI KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA ENEO LA MAFUTA NA GESI MANGAPWANI

Mamlaka ya Udhibiti Wa Huduma ya Maji Na Nishati Zanzibar (ZURA) imeshiriki katika kutangaza fursa za uwekezaji wa mafuta na gesi katika eneo la Mangapwani ikiwa ni miongoni mwa wadau wa nishati Zanzibar.

Fursa hizo zimetangazwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Wawekezaji wa ndani na wa nje ya nchi kwa lengo la kuibua wigo wa kukuza maendelea na upatikanaji endelevyo wa nishati Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Ndg. Sharif Ali Sharif aliwasisitiza waandishi wa habari kutoa taarifa hizo kwa wawekezaji juu ya swala zima la matumizi na mipango ya eneo la Mangapwani.

Eneo la Mangapwani linatarajiwa kuwa moja kati ya maaeneo ya uwekezaji kwa Sekta kiuchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta za Mafuta na Gesi pamoja na kuhakikisha eneo hilo linakua na ufanisi wa hali ya juu.