ZURA YABAINI UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA MAJI WILAYA YA KASKAZINI ‘A’ UNGUJA.

ZURA YABAINI UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA MAJI WILAYA YA KASKAZINI ‘A’ UNGUJA.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imekagua miundombinu ya Maji katika Kijiji cha Kiashange kilichopo Matemwe, Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja na kukutana na changamoto ya kung’olewa kwa Milango na Mabati katika vyanzo vya Maji.

ZURA imebaini Visima viwili (2) vimeng’olewa milango, Kisima kimoja (1) kimetolewa Paipu na Kisima kimoja (1) kimewekewa jiwe kwenye Paipu ya kupelekea Maji na kuzuia Huduma ya Maji kwenda katika maeneo yaliyokusudiwa, badala yake baadhi ya Watu hutumia Maji hayo yanayomwagika kunyweshea Wanyama wao.

Wananchi wa eneo hilo wamesikitishwa sana na kadhia hiyo na kuwaomba wananchi wenzao kulinda na kutunza miundombinu ya vyanzo vya maji hiyo kwani ndio inayowasaida kupata huduma ya maji safi na salama.

Aidha, ZURA imeitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuimarisha ulinzi imara na kuhakikisha miundombinu inalindwa ipasavyo kwa muda wote.

Pia, ZURA imesisitiza kuwa itahakikisha ulinzi katika vyanzo vya Maji unaimarishwa ili kuvilinda ipasavyo vyanzo hivyo na kuzuia kutokea uharibu kama huo.

ZURA hufanya ukaguzi wa vyanzo na miundombinu ya Maji mara kwa mara Unguja na Pemba ili kuhakikisha Huduma ya Maji inayotolewa inakua katika hali ya usalama zaidi.