ZURA NA EWURA YAFANYA KIKAO KAZI KUPANGA BEI ZA MAJI NA UMEME

ZURA NA EWURA YAFANYA KIKAO KAZI KUPANGA BEI ZA MAJI NA UMEME

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya Kikao kazi na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ili kubadilishana uzoefu wa upangaji wa bei za Maji na Umeme kufuatia mabadiliko ya mifumo ya utendaji kazi wa Mamlaka hizo.

Mkurugenzi Mkuu – ZURA Ndg. Omar Ali Yussuf wakati akifungua kikao kazi hicho alieleza ZURA inategemea kuanza rasmi udhibiti wa huduma za Umeme na Maji hivyo basi kikao kazi hicho kitatoa fursa nzuri ya kujadiliana namna bora ya upangaji wa bei hizo.

Aidha, Mkurugenzi Maji – EWURA Mha. Exaud Fetali Maro alieleza kua ushirikiano baina ya ZURA na EWURA utasaidia kubadilishana uzoefu wa udhibiti wa huduma za Maji na Nishati kwa kwa vile Mamlaka hiyo imepiga hatua katika udhibiti kwa upande wa Tanzania Bara.

Kikao hicho kilichofanyika kuanzia Tarehe 21/08/2023 hadi Tarehe 24/08/2023 katika ofisi za ZURA Maisara na kiliweza kujadili namna gani upangaji wa Bei za Maji na Umeme kutokana na uzoefu walionao katika kudhibiti huduma hizo.