ZURA YATOA MSAADA WA VITENDEKEA KAZI KWA WASAIDIZI WA SHERIA ZANZIBAR.

ZURA YATOA MSAADA WA VITENDEKEA KAZI KWA WASAIDIZI WA SHERIA ZANZIBAR.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetoa msaada wa vitendea kazi kwa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

Vitendea kazi hivyo vilikabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu (ZURA) Ndg. Omar Ali Yussuf kwa lengo kusambazwa kwa Wasaidizi wa Sheria Zanzibar katika Wilaya zote Unguja na Pemba.

Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi Idara ya Katiba na Msaada wa Sheria Ndg. Hanifa Ramadhan Said alieleza lengo la vifaa hivyo ni kusaidia jamii kupatiwa msaada wa kisheria hasa ikizingatiwa msaada huo hutolewa bila ya malipo na Maafisa waliopo kila Wilaya.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na ‘Printers’ kumi na moja (11), ‘Laptops’ tano (5) na ‘Tablets’ mbili (2) ambavyo vyote vina thani ya Shilingi Milioni Ishirini na Saba (27,000,000/-)