BEI MPYA ZA MAFUTA ZATANGAZWA 

BEI MPYA ZA MAFUTA ZATANGAZWA 

Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Ndg. Mbarak Hassan Haji ametangaza Bei Mpya za Mafuta Leo Tarehe 08/08/2023 katika Ukumbi wa ZURA, Maisara Unguja.

Bei hizo zilizotangazwa Leo zitaanza kutumika rasmi kuanzia Kesho Siku ya Jumatano Tarehe 09/08/2023 ni:

  • PETROLI: TZS 2,970/LITA
  • DIZELI: TZS 2,843 LITA
  • MAFUTA YA TAA: TZS 2,921 LITA
  • MAFUTA YA NDEGE: TZS 2,365 LITA

Sababu za mabadiliko hayo ni kuongezeka kwa Bei za Mafuta katika Soko la Dunia na mabadiliko ya thamani ya Shilingi ya Tanzania kwa Dola za Marekani.

Mamlaka hupanga na kutangaza Bei za Mafuta Tarehe 8 ya kila Mwezi kwa kuzingatia Bei zifuatazo:

  • Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations).
  • Gharama za uingizaji Mafuta katika Bandari ya Dar-es-Salaam na Tanga.
  • Thamani ya Shilingi ya Tanzania kwa Dola za Kimarekani.
  • Gharama za Usafiri, Bima na ‘Premium’ hadi Zanzibar.
  • Kodi na Tozo za Serikali.
  • Kiwango cha faida kwa Wauzaji wa Jumla na Reja Reja.
347 downloads 1.0 Rahma Thabit 14-08-2023 7:49