MKURUGENZI MKUU – ZURA ATEMBELEA MAONESHO 

MKURUGENZI MKUU – ZURA ATEMBELEA MAONESHO 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Ndg. Omar Ali Yussuf ametembelea Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) yanayoendelea Dole – Kizimbani, Zanzibar tangu Tarehe 01/08/2023 mpaka Tarehe 10/08/2023.
Mkurugenzi Omar ametembelea mabanda tofauti yakiwemo banda la  Wakulima, Kampuni ya Oryx na Kamisheni ya Utalii, pamoja na Mabanda ya Wajasiriamali waliojitokeza kushiriki katika Maonesho hayo.
Mkurugenzi huyo amepata nafasi ya kuelewa njia tofauti za kilimo cha umwagiliaji na aina ya umwagiliaji katika kilimo ikiwemo ufungaji wa ‘Drip’ kwa mimea, upigaji bomba kutoka katika kianzio cha Maji moja kwa moja pamoja na uhifadhi maji katika mahodhi maalum.
Aidha, katika matembezi hayo Mkurugenzi Omar alisikiliza changamoto zinazowakabili Wakulima hao ikiwemo ni upatikanaji wa Maji kutokua wa uhakika na kupekea changamotoa katika Kilimo cha umwagiliaji, ambapo inaweza kuwa fursa nzuri kwa uwekezaji katika sekta hiyo.
Mamlaka inahamasisha wawekezaji katika sekta ya kilimo juu ya uvunaji wa maji ya mvua na kuyahifadhi kwa lengo la kutumika katika umwagiliaji badala ya kutumika visima na maji ya mabomba na kujenga miundombinu rafiki ya umwagiliaji.