ZURA YASHIRIKI MAONESHO

ZURA YASHIRIKI MAONESHO

ZURA YASHIRIKI MAONESHO

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati imeshiriki maonesho ya kilimo (Nane Nane) yanayofanyika kizmbani Zanzibar kuanzia Tarehe 01/08/2023 mpaka Tarehe 10/08/2023.

Ushiriki wa maonesho hayo utaipa Mamlaka fursa ya kuweza kutoa elimu kwa wadau wake wote watakaotembelea katika banda la Mamlaka na kuweza kujua juu ya huduma zinazodhibitiwa zikiwemo Maji, Umeme, Mafuta pamoja na gesi ya Kupikia (LPG). Wananchi hao pia watapata uwelewa wa matumizi sahihi na salama ya huduma hizo.

Aidha, pamoja na elimu inayotolewa kwa wananchi katika maonesho hayo pia Mamlaka itapata fursa nzuri ya kuongeza idadi ya wawekezaji katika Sekta za Maji na Nishati kwa vile wawekezaji hao hutembelea na kuweza kujua juu ya uekezaji katika sekta hizo.

Mamlaka inahamasisha wawekezaji katika sekta ya kilimo juu ya uvunaji wa maji ya mvua na kuyahifadhi kwa lengo la kutumika katika umwagiliaji badala ya kutumika visima na maji ya mabomba na kujenga miundombinu rafiki ya umwagiliaji.

ZURA imekua ni miongoni mwa washiriki katika maonesho ya kilimo (Nane Nane) katika maadhimisho ya siku ya wakulima ambayo huadhimishwa Tarehe 8 Mwezi 8 kila mwaka, ikizingatiwa kuwa wadau wengi katika sekta ya kilimo ni wakulima wa umwagiliaji (irrigation).