ZURA YAKUTANA NA WADAU WA GESI.

ZURA YAKUTANA NA WADAU WA GESI.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya kikao na wadau wa Gesi kwa lengo la kujadili muongozo wa ujenzi wa miundombinu ya gesi ya kupikia (LPG), Kilichofanyika katika ofisi za ZURA maisara, Siku ya Alhamis ya Tarehe 27/07/2023 na Siku ya Ijumaa ya Tarehe 28/07/2023.

Kikao hicho cha kujadili Muongozo huo kilishirikisha wawakilishi kutoka Kampuni za Gesi na Taasisi za Serekali zikiwemo Taifa Gas, Oilcom, Oryx Gas, V-Gas, ZAWA, ZAWEMA, Kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU). Aidha kikao hicho kiliwataka wadau kutoa mapendekezo, maoni, pamoja na njia nzuri za kuboresha miundombinu hiyo.

Aidha, Muongozo huo umeandaliwa ili kuwasiadia wawekezaji kupata maelezo ya kina ya namna bora ya ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhia na kujazia gesi ya kupikia (LPG) katika mitungi inayouzwa na kusambazwa majumbani.

Msaidizi Meneja wa Divisheni ya Mafuta ZURA Ndg. Yahya Abdulhamid Yahya amewaeleza wadau hao kuepuka kujenga vituo hivyo vya kuhifadhia mitungi ya gesi karibu na huduma za kijamii.

Mamlaka inakawaida ya kuitisha kikao cha wadau wake kila inapoandaa miongozo ili kukusanya maona na mapendekezo ya wadau wake.