ZURA NA UWEKEZAJI

ZURA NA UWEKEZAJI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imelenga kuongeza idadi ya wawekezaji katika Sekta za Maji na Nishati kwavile wawekezaji wengi hutembelea na kuelezwa fursa za uwekezaji katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba Temeke, Dar es salam kuanzia Tarehe 28/06/2024 mpaka Tarehe 13/7/2024.

Ushiriki wa Mamlaka katika Maonesho hayo pia hutoa fursa ya kutoa elimu kwa wadau wake wanaotembelea katika banda lake kujifunza kuhusu udhibiti wa sekta ya Maji, Umeme, Mafuta na Gesi.

Maonesho ya 48 ya Biashara Dar es salaam (Sabasaba) yameandaliwa na Mamlaka ya Biashara Tanzania (TanTrade) na kwa upande wa Jengo la Zanzibar ambamo Mamlaka inapatikana yanasimamiwa na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar ili kutoa fursa kwa Tasisi za Serekali, Binafsi na Wajasiriliamali kuonesha, kutangaza na kuuza bidhaa zao kwa Wananchi.

Miongoni mwa Washiriki wa Maonesho haya kutoka Zanzibar ni pamoja na ZURA, ZAA, ZRA, ZBS, ZPDC, ZPC, PBZ, ZCT, BPRA, ZAIDAT, Refasha, ZanFast Ferries na Wajasiriamali.v

Maonesho ya Sabasaba ya Mwaka huu 2024 yamejumuisha Kampuni zaidi ya elfu tatu na mia tano (3,500) kutoka nchi zaidi ya thelathini na tano (35) na yamefunguliwa rasmi Leo na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.